Waraka wa pili kwa Wakorintho

Waraka wa pili kwa Wakorintho ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Ni kati ya barua mbili zilizomo za Mtume Paulo kwa Wakristo mjini Korintho (Ugiriki).
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Mazingira
[hariri | hariri chanzo]Mdo 19:21-20:1 inasimulia Paulo alivyohama Efeso kutokana na matatizo kuzidi, akaelekea Makedonia na Ugiriki.
Toka huko alipata nafasi ya kuhubiri katika Iliriko, yaani kuanzia Albania ya leo kwenda kaskazini (Rom 15:19).
Wakati huo alipata habari mbaya kuhusu Wakorintho, akawaandikia tena na tena kabla hajawaendea kwa mara ya tatu.
Mpangilio
[hariri | hariri chanzo]Labda kwa kuwa ni mshono wa barua hizo mbalimbali, mpangilio wa 2Kor haueleweki, ingawa ina salamu na shukrani mwanzoni, na salamu nyingine mwishoni kama kawaida.
Katikati mada kuu ni tatu: kujitetea, mchango na mashambulizi dhidi ya wapinzani.
Barua hiyo inatusaidia hasa kumjua Paulo mwenyewe (2Kor 11:1-12:13).
Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- C. MHAGAMA, Baba Paulo, Mtume wa Kimataifa - ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1989, ISBN 9976-67-028-1
- W. NGOWI, O.F.M.Cap, Paulo na Nyaraka Zake, ed. Salvatorianum, Morogoro 1999 – ISBN 9987-645-02-X
- J. MALUNDA, Paulo Mtume na Yesu Kristo wake, ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 2001, ISBN 9976-67-153-9
- WABENEDIKTI WA NDANDA, Tufikirie Waraka wa Pili wa Mtume Paulo kwa Wakorinti, ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1990 – ISBN 9976-63-233-9
Marejeo ya lugha nyingine
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Tafsiri ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]Vingine
[hariri | hariri chanzo]| Wikisource has original text related to this article: |

- . Encyclopædia Britannica. Juz. la 7 (tol. la 11th). 1911. ku. 150–154.
{{cite encyclopedia}}: Cite has empty unknown parameter:|coauthors=(help)
Online translations of Second Epistle to the Corinthians:
- Online Bible at GospelHall.org
- Commentary articles by J. P. Meyer on Second Corinthians, by chapter: 1–2 Ilihifadhiwa 15 Juni 2009 kwenye Wayback Machine., 3 Ilihifadhiwa 16 Juni 2009 kwenye Wayback Machine., 4:1–6:10 Ilihifadhiwa 16 Juni 2009 kwenye Wayback Machine.,
- 6:11–7:16 Ilihifadhiwa 16 Juni 2009 kwenye Wayback Machine.,
- 8–9 Ilihifadhiwa 16 Juni 2009 kwenye Wayback Machine., 10–13 Ilihifadhiwa 16 Juni 2009 kwenye Wayback Machine.
| Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waraka wa pili kwa Wakorintho kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |