Alida Chelli

Alida Rustichelli (23 Oktoba 1943 – 14 Desemba 2012), alifahamika kitaaluma kwa jina la Alida Chelli (matamshi ya Kiitalia: [aˈliːda ˈkɛlli]), alikuwa mwimbaji na mwigizaji kutoka Italia, alijulikana zaidi kwa kushiriki katika maonyesho ya muziki jukwaani.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Maisha ya awali na kazi yake
[hariri | hariri chanzo]Alikuwa binti wa mtunzi wa muziki Carlo Rustichelli na dada wa mtunzi wa muziki Paolo Rustichelli. Alipata mafanikio yake ya kwanza kama mwimbaji kupitia wimbo “Sinnò me moro”, unaofungua filamu ya mwaka 1959 The Facts of Murder.
Baadae, Chelli alipata umaarufu mkubwa jukwaani, akicheza katika vichekesho kadhaa vya muziki vilivyofanikiwa, kama vile Rugantino (1978), akiwa pamoja na Enrico Montesano; Cyrano (1979), akiwa pamoja na Domenico Modugno; na Aggiungi un posto a tavola (1990), akiwa pamoja na Johnny Dorelli.
Pia alishiriki katika filamu kadhaa, hasa za vichekesho, na vipindi vya televisheni.[1][2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.imdb.com/name/nm0155072/
- ↑ https://www.discogs.com/artist/618714-Alida-Chelli?redirected=true
| Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Alida Chelli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |