Anna Netrebko

Anna Yuryevna Netrebko (amezaliwa 18 Septemba 1971)[1] ni mwimbaji wa soprano wa opera wa Urusi ambaye ametumbuiza katika Matamasha ya Salzburg, Metropolitan Opera, Vienna State Opera, Royal Opera, na La Scala.[2]
Maisha ya awali na mafunzo
[hariri | hariri chanzo]Netrebko alizaliwa huko Krasnodar katika familia yenye asili ya Kuban Cossack. Wakati akisoma katika Chuo cha Muziki cha Saint Petersburg (Saint Petersburg Conservatory), Netrebko alifanya kazi kama mfagiaji na mfanya usafi (janitor) katika Ukumbi wa Michezo wa Mariinsky huko Saint Petersburg. [3]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Chini ya uongozi wa Gergiev, mnamo 1994 Netrebko alicheza kwa mara ya kwanza jukwaani kama mwimbaji wa opera katika ukumbi wa Mariinsky akiwa na umri wa miaka 22 kama Susanna katika mchezo wa The Marriage of Figaro, licha ya kwamba hapo awali alikuwa amepangwa kucheza kama Barbarina.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.britannica.com/biography/Anna-Netrebko
- ↑ https://annanetrebko.com/about/
- ↑ https://www.allmusic.com/artist/anna-netrebko-mn0000032526
- ↑ https://open.spotify.com/artist/5moBlpk9BYtujdRW6VLepL
| Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Anna Netrebko kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |