Nenda kwa yaliyomo

Jared Leto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jared Leto

Jared Joseph Leto (alizaliwa 26 Desemba 1971) ni muigizaji na mwanamuziki wa Marekani. Anajulikana kwa mtindo wake wa uigizaji wa kuvaa kikamilifu tabia ya mhusika (method acting)[1] katika uhusika mbalimbali, na amepokea tuzo na heshima mbalimbali katika kazi yake iliyodumu kwa miongo mitatu, ikiwa ni pamoja na Tuzo ya Academy (Oscar) na Tuzo ya Golden Globe. Pia, yeye ni kiongozi na mwimbaji mkuu (frontman) wa bendi ya muziki wa rock ya Thirty Seconds to Mars.[2]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Jared Joseph Leto alizaliwa mnamo Desemba 26, 1971,[3] huko Bossier City, Louisiana, kwa mama yake Constance Leto (jina la utotoni Metrejon). Mama yake ana asili ya Kikajuni (Cajun). Leto ni jina la ukoo la baba yake wa kambo.[4]

Mnamo mwaka 1992, Leto alihamia Los Angeles ili kuendeleza taaluma ya uigizaji. Katika mwaka huo huo, Leto alifanya utambulisho wake wa kwanza wa filamu ya televisheni akiigiza pamoja na Alicia Silverstone katika Cool and the Crazy, na akapata nafasi yake ya kwanza ya filamu katika tamthilia ya mwaka 1995 ya How to Make an American Quilt. Baadaye aligiza pamoja na Christina Ricci katika The Last of the High Kings (1996) na akapata nafasi ya usaidizi katika Switchback (1997).[5]

  1. ↑ https://web.archive.org/web/20140202164421/http://www.mvff.com/jared-leto-editorial/
  2. ↑ https://www.ocregister.com/2013/10/09/thirty-seconds-to-mars-rises-to-new-heights/
  3. ↑ https://www.tribute.ca/people/jared-leto/2203/
  4. ↑ https://www.telegraph.co.uk/culture/film/3575916/Not-just-a-pretty-face.html
  5. ↑ https://www.rogerebert.com/festivals/prefontaine-premieres-at-sundance
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jared Leto kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.