Nenda kwa yaliyomo

Phil Thompson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Phil Thompson

Philip Bernard Thompson (alizaliwa 21 Januari 1954) ni mchezaji wa zamani wa soka kutoka Uingereza aliyekuwa akicheza katika nafasi ya beki.

Alicheza kwa Liverpool katika miaka ya 1970 na 1980. Katika kipindi hicho, pia aliwakilisha timu ya taifa ya Uingereza mara 42, na aliwahi kuwa nahodha wa England mara sita.

Baada ya kustaafu kucheza soka, Thompson aliendelea kuitumikia Liverpool akiwa kocha msaidizi. Katika msimu wa 2001–02, alihudumu pia kama kocha wa muda kwa kipindi cha miezi sita wakati kocha mkuu Gérard Houllier alipokuwa mgonjwa.

Kazi ya Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Thompson aliichezea timu ya taifa ya Uingereza katika jumla ya mechi 42 kati ya 1976 na 1982.

Akiwa na umri wa miaka 22, alicheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa tarehe 24 Machi 1976, ambapo England iliifunga Wales 2–1 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Racecourse, Wrexham.[1][2]

  1. ↑ https://www.liverpoolfc.com/info/phil-thompson
  2. ↑ https://web.archive.org/web/20151124141813/http://www.fifa.com/fifa-tournaments/players-coaches/people=58935/index.html
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Phil Thompson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.