Nenda kwa yaliyomo

Verna Vels

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Verna Barbara Robertson Vels (13 Juni 1933 - 21 Agosti 2014) alikuwa mwandishi na mtangazaji wa redio na televisheni kutoka nchini Afrika Kusini. Alikuwa na kazi ya programu za sanaa na programu zinazohusu vijana. Alihusika kwa karibu katika kupanga programu za televisheni kwa ajili ya kuanzisha huduma ya Kiafrikana na akaanzisha jarida la watoto. Kazi yake maarufu zaidi ilikuwa Liewe Heksie; hadithi hizo ziliandikwa awali kwa ajili ya redio na baadaye kuchapishwa na kuhaririwa kwa ajili ya televisheni na video. [1]

Verna Vels alizaliwa Reitz, Orange Free State, nchini Afrika Kusini. [2] Alisoma Chuo Kikuu cha Pretoria, na mwaka wa 1954 alimaliza shahada ya BA, alisomea Kiafrikana na Kiholanzi, Kiingereza, na Historia ya Sanaa.

Mnamo Desemba mwaka1954, alianza kufanya kazi kama mtangazaji wa redio katika SABC huko Durban, ambapo alivutiwa na vipindi vya watoto. Mnamo mwaka 1963, alihamia Johannesburg. Mnamo mwaka 1968 alifanya kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja katika Radio Netherlands huko Hilversum Wereldomroep. Mnamo mwaka 1973 alihamia Durban na kuwa mratibu wa Vipindi vya Kiafrikana huko Natal na kuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa kama mratibu katika eneo hilo. Mnamo 1mwaka 974, Vels alirudi Johannesburg, ambapo aliteuliwa na Televisheni kama mratibu wa jarida la Kiafrikana lililokuwa vipindi vya watoto. Vipindi kama vile Kraaines na Wielie Walie vilitengenezwa chini ya mwongozo wake. Kwa miaka yote ya uwepo wake, alitoa sauti ya Bennie Wielie Walie kama msomaji wa vitabu. Katika miaka miwili kabla ya Televisheni kurushwa rasmi (tarehe 5 Januari mwaka 1976), Vels alihusika katika uzalishaji na upangaji wa vipindi na hatimaye katika ununuzi wa vipindi katika nchi za kigeni. Alianza kuandika kwa ajili ya redio mapema katika taaluma yake, na sehemu kubwa ya kazi hii hatimaye ilichapishwa.

Hadithi ya kwanza ya Liewe Heksie (Mpenzi mchawi mdogo) zilitangazwa kwenye redio mwaka wa 1961. Mfululizo kadhaa wa Liewe Heksie ulirushwa hewani.

Vitabu vya kwanza vya "Liewe Heksie" vilichapishwa mwaka wa 1965 na wachapishaji Human & Rousseau. Kwa miaka mingi, jumla ya vitabu 10, makala nane, na CD, video, na DVD nyingi zilitolewa. Kitabu cha hivi karibuni kilikuwa kinaitwa "Liewe Heksie en die rekenaar" (Mpenzi mchawi mdogo na kompyuta) ambacho kilisomwa mwaka wa 1999 (kilichochorwa na Piet Grobler). Liewe Heksie kilianza kuchapishwa kwenye televisheni mwaka wa 1978 na katika mfululizo wa vipindi 26. Mfululizo wa pili uliofuata wa mwaka wa 1981. Kwa mfululizo wa jumla ya vipindi 52 vya televisheni, alihariri hadithi za zamani na kuandika hadithi mpya. Mfululizo huo pia ulisababisha idadi ya vitabu vyenye vielelezo kutoka kwenye televisheni. Liewe Heksie pia alionekana katika tasni ya uigizaji kwa watoto katika kumbi kama vile ukumbi wa michezo wa Nico Malan huko Cape Town, Ukumbi wa michezo wa Sand du Plessis huko Bloemfontein na Ukumbi wa michezo wa State huko Pretoria. Vels pia aliandika tamthilia za Liewe Heksie za "Klein Karoo Nasionale Kunstefees" na Idara ya Maigizo ya Chuo Kikuu cha Pretoria kuadhimisha kumbukumbu ya miaka thelathini.

Vels aliandika riwaya ianayohusu vijana, Alet, mwaka wa 1965 kwa ajili redio; ilichapishwa mwaka wa 1978 na Perskor-Publishers. Alipanga tamthilia kadhaa za redio, na alifanya uandishi wa mwanzo kwa ajili ya vipindi vya redio. Tamthilia ya asili kama ile ya Little-Theatre ya zamani pamoja na Helen wa Troy Clemens na Uncle Bob na hadithi ya mwisho. Ilitangazwa mara mbili. Mnamo Februari mwaka 1983, alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Programu ya TV1 ya (Kiafrikana) nafasi ya juu zaidi kuwahi kushikiliwa na mwanamke katika miaka hiyo. Baada ya marekebisho kadhaa ndani ya SABC, ilishikilia nafasi zingine kadhaa na kustaafu mwaka wa 1993 baada ya kazi ya karibu miaka minne katika redio na televisheni.

Alipokea tuzo kadhaa kutoka Taasisi za Utamaduni, ikiwa ni pamoja na:

  • Die Federasie van Rapportryerskorpse kwa machapisho ya Liewe Heksie-Family (1985).
  • Nishani ya Heshima kwa Maendeleo ya Utamaduni ya Wanawake (1993).
  • Artes wa SABC kwa michango yake katika Utangazaji.
  • FAK kwa ajili ya kukuza Sanaa za Maonyesho (1996).
  • Tuzo ya CP Hoogenhout kwa Watoto wa UNISA (2002).

Verna Vels alifariki kwa ugonjwa wa saratani Alhamisi, Agosti 21, 2014, akiwa na umri wa miaka 81. [3]

  • Die Groot Liewe Heksie-Storieboek (miaka ya 1970), iliyochorwa na Dorothy Hill,
  • Hadithi za Lekker Liewe Heksie (miaka ya 1970), zilizochorwa na Dorothy Hill,
  • Liewe Heksie en die rugbywedstryd (1988), iliyochorwa na Nikki Jones,
  • Liewe Heksie en die rekenaar (1999), iliyochorwa na Piet Grobler,
  • Liewe Heksie Omnibus (2002), kwa picha na Piet Grobler, [4]
  1. ↑ "Verna Vels | Who's Who SA". whoswho.co.za (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-03-17. Iliwekwa mnamo 2018-01-11.
  2. ↑ "StorieWerf biography of Verna Vels" (kwa Afrikaans). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-11-04. Iliwekwa mnamo 2026-04-01.{{cite web}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
  3. ↑ "Liewe Heksie creator Verna Vels dies from cancer". IOL.co.za. Iliwekwa mnamo 24 Agosti 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. ↑ Vels, Verna (2002). Liewe Heksie Omnibus (kwa Kiafrikana) (tol. la 1st). Kaapstad: Human & Rousseau (Pty) Ltd. ISBN 9780798142212.